Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 20:30

Afya ya Mandela yazorota


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela nyumbani kwake Qunu, akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake Julai 18, 2012.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela nyumbani kwake Qunu, akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake Julai 18, 2012.

Familia yakutana kujadilia hali ya afya ya Madiba huku askofu mkuu akimwombea amani katika siku zake za mwisho.

Rais wa Afrika Kusini Jacob zuma ameahirisha safari yake ya Msumbiji wakati rais wa zamani Nelson Mandela akiwa bado katika hali mbaya ya afya katika hospitali moja mjini Pretoria. Madaktari wanasema rais huyo wa zamani amewekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Kiongozi huyo wa zamani ambaye alipigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo amelazwa katika hospitali kwa takriban wiki tatu sasa kutokana na maambukizo ya mapafu.

Askofu mkuu wa Capetown Thabo Makgoba Jumanne aliongoza maombi ya bwana Mandela rais wa kwanza mweusi na kutakia amani na utulivu katika siku zake za mwisho.

Jamii ya bwana Mandela imekusanyika katika nyumba yake katika kijiji cha Qunu mashariki mwa jimbo la Cape na vyombo vya habari vya Afrika Kusini vinaripoti kwamba watoto wake waliitisha mkutano ili kujadili masuala muhimu ya kifamilia.

Rais wa Marekani Barack Obama anategemewa kuwasili Afrika Kusini Ijumaa hii kama sehemu ya ziara yake ya wiki nzima barani Afrika. Atatembelea kisiwa cha Robben ambako bwana Mandela alifungwa jela kwa miaka 27.
XS
SM
MD
LG