Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 22:52

viongozi wa Afrika watakiwa kukumbatia demokrasia


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akionyesha hati ya kiapo baada ya sherehe za kumuapisha zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi, April 9, 2013.

Wanaharakati wa demokrasia wanatoa shinikizo kwa utawala wa kiimla barani Afrika kukumbatia demokrasia. Wameahidi kuendelea kuunga mkono jamii za kiraia na makundi ya kufatilia uchaguzi barani Afrika.

Katika wiki chache zijazo Tanzania itaungana na Ivory Coast, Guinea na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika zoezi la uchaguzi mkuu katika nchi hizo.

Mkurugenzi wa Afrika katika taasisi ya National Endowment for Democracy yenye makao yake Washington DC, Dave Peterson anasema chaguzi huru na za haki ni vyema zijumuishe uwazi, uwajibikaji na utawala mzuri. Jambo ambalo haliko hivyo siku zote.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:06:24 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bw. Peterson anasema wapiga kura nchini Nigeria na Senegal wamekuwa na mazoea ya kupiga kura, ingawaje baadhi ya watu katika nchi hizo wanadai hakuna utawala mzuri. Kwa upande mwingine, anasema watalaamu wa maendeleo wanasema Ethiopia na Rwanda zinatawaliwa vizuri, ingawaje watala wao hawastahmili uasi na upinzani ambao ni mdogo sana au hauonekani hadharani.

Taasisi hii ya demokrasia na makundi mengine yanayounga mkono demokrasia yanasema lengo lao kuu ni kuongeza kiwango cha ushiriki wa kidemokrasia katika chaguzi.

XS
SM
MD
LG