Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:27

Marekani na Saudi Arabia wanahimiza tena mazungumzo ya kusitisha mapigano Sudan


Jengo la huduma ya afya ni miongoni mwa majengo yaliyoharibiwa kufuatia mapigano nchini Sudan. June 1, 2023.
Jengo la huduma ya afya ni miongoni mwa majengo yaliyoharibiwa kufuatia mapigano nchini Sudan. June 1, 2023.

Marekani na Saudi Arabia siku ya Jumapili wamehimza tena haja ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya majenerali wa kijeshi wa Sudan wakati mapigano yakiendelea katika wiki yake ya nane.

Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yamefikiwa na kuvunjwa, na Marekani iliwawekea vikwazo majenerali wawili wanaohasimiana wiki iliyopita ikizilaumu pande zote mbili kwa umwagaji damu wa kusikitisha.

Wajumbe wa jeshi la Sudan na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) wamesalia katika mji wa pwani wa Saudi Arabia wa Jeddah licha ya kuvunjika kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano, wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imesema.

Wapatanishi wa kigeni wametoa wito kwa pande zote kukubaliana na kutekeleza kwa ufanisi usitishaji mpya wa mapigano kwa lengo la kupatikana makubaliano ya kudumu ya kusitisha uhasama, wamesema maafisa mjini Riyadh.

Forum

XS
SM
MD
LG