Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:44

Madagascar yatinga nusu fainali ya CHAN


Washabiki wa Senegal wakionyesha mbwe mbwe zao.

Washiriki  wa mara ya kwanza katika michuano ya CHAN Madagascar walitinga nusu fainali ya michuano hiyo ya TotalEnergies African Nations Championship (CHAN) 2022 nchini Algeria baada ya kuwalaza Msumbiji 3-1 katika mchezo wa kusisimua siku ya Jumamosi.

Washiriki wa mara ya kwanza katika michuano ya CHAN Madagascar walitinga nusu fainali ya michuano hiyo ya TotalEnergies African Nations Championship (CHAN) 2022 nchini Algeria baada ya kuwalaza Msumbiji 3-1 katika mchezo wa kusisimua siku ya Jumamosi.

Timu hiyo ijulikanayao kama Barea walionyesha kandanda safi katika Uwanja wa Chahid Hamlaoui mjini Constantine siku ya Jumamosi wakithibitisha kwamba maendeleo yao katika michuano hiyo hayajawa ya bahati.

Solomampionona Koloina Razafindranaivo alifunga bao la kuongoza dakika ya 18 baada ya kuingia kwenye eneo la hatari upande wa kulia na kupeleka shuti la nguvu la mguu wa kushoto hadi wavuni. Kipa wa Msumbiji Victor hakuweza kufanya lolote kuzuia shuti hilo.

Madagascar walidhibiti kasi ya mchezo na kuwashambulia Mambas wa Msumbiji mara kadhaa na katika dakika ya 42, shambulio lao nusura lizae matunda pale Tokinantenaina Olivier Randriatsiferana anayejulikana kama Tsiry alipofanya shambulizi kwenye eneo la hatari na kuuwekea mpira kwa Jean Yvon Razafindrakoto ambaye akiwa ana kwa ana na golikipa Victor alishindwa kuweka mpira wavuni.

Msumbiji walijaribu kurejesha utulivu wao lakini walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0. Madagascar walianza kipindi cha pili kutoka pale walipoishia kipindi cha kwanza kwa kupeleka mashambulizi mengo langoni kwa Msumbiaji wakafanikiwa katika dakika ya 67 wakati Jean Razafindrakoto alipofunga bao la pili.

Marcio Ravelomanantsoa alikamilisha safari ya virago ya Msumbiji baada ya kupachika bao la tatu katika dakika ya 87. Na bao pekee la kufutia machozi la Msumbiji lilifungwa na Isac Decarvalho.

Madagascar sasa wametinga nusu fainali ya CHAN kwa mara ya kwanza na watamenyana na Simba wa Teranga- Senegal ambao waliilaza Mauritania 1-0 siku ya Ijumaa mjini Annaba.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG