Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 07:34

Chama kipya cha upinzani Lesotho kinaonekana kinaongoza viti vingi bungeni


Raia mwanamke wa Lesotho akipiga kura katika moja ya vituo vya upigaji kura vilivyopo nje ya mji mkuu wa Maseru.
Raia mwanamke wa Lesotho akipiga kura katika moja ya vituo vya upigaji kura vilivyopo nje ya mji mkuu wa Maseru.

Chama kilichoanzishwa hivi karibuni kinachoongozwa na mfanyabiashara milionea wa Almasi kilionekana Jumapili kushinda uchaguzi wa bunge wa Lesotho kikiwa kimepata kiasi cha kutosha ya wingi mdogo kulingana na matokeo ya awali kutoka kwa tume ya uchaguzi.

Kufikia Jumapili alasiri matokeo ya kura iliyopigwa Oktoba 7 yalikuwa kutoka maeneo 49 kati ya jumla ya maeneo bunge 80. Chama cha Revolution for Prosperity (RFP) kilichoundwa na Sam Matekane mwezi Machi kilikuwa kimepata viti 41 kiwango cha chini kinachohitajika kuwa na wingi mdogo.

Chama tawala kilichopo madarakani cha All Basotho Convention (ABC) ambacho kinaendesha nchi hiyo yenye watu milioni 2.14 tangu mwaka 2017 kilifanya vibaya na kukosa viti vyovyote hadi sasa hesabu ilionyesha hivyo.

Chama cha Democratic Congress (DC) ambacho ni chama kikuu cha upinzani na mwanachama katika serikali ya muungano kimeshika nafasi ya pili kwa RFP katika kinyang'anyiro hicho baada ya kupata viti visivyopungua sita.

XS
SM
MD
LG