Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kwa niaba ya Marekani amewapongeza watu wa Uganda kwa maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa nchi hiyo pamoja na maendeleo makubwa yaliyopatikana yenye mafanikio katika nchi tangu wakati huo.
Kwa miongo kadhaa, watu wa Marekani na wa Uganda wameshirikiana kwa manufaa ya nchi zao zote mbili, hasa kwa afya ya umma na kimataifa. Tunashukuru pia jukumu la uongozi ambalo Uganda imetekeleza katika amani na usalama wa kikanda kupitia ushiriki wake mkubwa katika operesheni za kulinda amani na sera yake ya kuwakaribisha wakimbizi.
Marekani inatarajia kuwepo miaka mingi zaidi ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili kati ya nchi hizo.