Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:13

Wachunguzi wa UN wametoa ripoti inayoshutumu ukiukaji wa haki za binadamu Libya


Nembo ya Umoja wa Mataifa katika kitengo kinachohusika na masuala ya haki za binadamu
Nembo ya Umoja wa Mataifa katika kitengo kinachohusika na masuala ya haki za binadamu

Ripoti mbaya iliyotolewa na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Libya inaishutumu serikali na makundi ya upinzani kwa kutenda ukiukaji mkubwa bila ya khofu ya kuadhibiwa ambapo huenda uhalifu mwingi dhidi ya ubinadamu. Ripoti hiyo itawasilishwa kwa baraza la haki za binadamu la umoja wa Mataifa siku ya Jumatano.

Hii ni ripoti ya tatu ya tume huru inayoangazia ukweli kuhusu Libya yenye wanachama watatu tangu ilipoanza kuandika madai ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo mwaka 2016. Wachunguzi wanaona kwamba Libya ni nchi isiyoheshimu sheria ambapo wahalifu wa uhalifu wa kimataifa hawawajibiki kwa matendo yao. Hitimisho hili linatokana na mamia ya mahojiano na mikusanyiko ya habari pamoja na ushahidi uliokusanywa kutoka vyanzo tofauti.

Ripoti ya hivi karibuni inahusisha kipindi cha kuanzia Machi hadi Juni. Wachunguzi waliangalia masharti ya kizuizini katika vituo rasmi 27 na vile, visivyo rasmi, ikiwa ni pamoja na magereza ya siri na yake ya ziada ya kisheria. Mwenyekiti wa misheni Mohamed Auajjar anasema uchunguzi umebainisha kwamba mifumo ya wazi ya ukiukaji wa haki za binadamu katika maeneo haya yote.

XS
SM
MD
LG