Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:55

Washington inamshutumu Rais wa Tunisia kwa kudumaza taasisi za kidemokrasia


Rais wa Tunisia, Kais Saied katika moja ya hotuba zake kwa taifa la Tunisia. Sept. 20, 2021.
Rais wa Tunisia, Kais Saied katika moja ya hotuba zake kwa taifa la Tunisia. Sept. 20, 2021.

Washington siku ya Alhamis ilimshutumu Rais wa Tunisia, Kais Saied kwa kudumaza taasisi za kidemokrasia za nchi hiyo baada ya kuwafukuza kazi majaji kadhaa huku kukiwa na safu ya hatua ambazo zilionekana kulenga kuunganisha utawala wa mtu mmoja.

Rais Saied ambaye pia amefanya mabadiliko kwenye nafasi ya tume huru ya uchaguzi na kusema kwamba atazindua katiba mpya mwezi huu aliwashutumu majaji hao kwa rushwa na kuwalinda magaidi katika hotuba yake kwa njia ya televisheni siku ya Jumatano.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Marekani, Ned Price alisema uondoaji huo ni sehemu ya mwenendo wa kutisha wa hatua ambazo zimedhoofisha taasisi huru za kidemokrasia nchini Tunisia.

Maafisa wa Marekani waliwasiliana na wenzao wa Tunisia kutathmini umuhimu wa kuangalia na kuleta uwiano katika mfumo wa kidemokrasia Price alisema wakati wa mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari.

XS
SM
MD
LG