Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:21

Mkuu wa zamani wa kijasusi Afrika kusini awasilisha mashtaka dhidi ya Rais Ramaphosa


Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa

Mkuu wa zamani wa kijasusi nchini Afrika kusini Arthur Fraser alisema Jumatano kwamba aliwasilisha malalamiko ya kisheria dhidi ya Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa akimtuhumu kuteka nyara na kuwahonga majambazi walioiba mamilioni ya dola kutoka kwa moja ya mali zake.

“Nimechukua hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa ya kufungua mashtaka ya jinai dhidi ya mheshimiwa, Rais wa Jamhuri ya Afrika kusini, Cyril Ramaphosa” mkuu wa zamani wa ujasusi Arthur Fraser alisema katika taarifa.

Kulingana na Fraser ni kwamba wezi hapo Februari tisa mwaka 2020 walivamia shamba kaskazini mwa Johannesburg mali ya Rais Ramaphosa kwa msaada wa mfanyakazi wa ndani ambapo walifanikiwa kuiba zaidi ya dola milioni nne.

Fraser amemshutumu Ramaphosa kwa kuandaa utekaji nyara wa washukiwa, kuhojiwa kwao kuhusu mali yake, pamoja na hongo. Rais Ramaphosa alificha uhalifu kwa idara ya huduma ya polisi ya Afrika kusini au idara ya mapato ya Afrika kusini na baada ya hapo akawalipa wahalifu kwa kukaa kwao kimya alisema mkuu huyo wa zamani wa kijasusi huko Afrika kusini, Arthur Fraser.

XS
SM
MD
LG