Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 05:33

DRC imekubali kuwaachia wanajeshi wawili inaowashikilia wa nchini Rwanda


Rais Félix Tshisekedi wa DRC (L) akiwa na mwenzake Rais wa Angola João Lourenço mjini Luanda, Angola. Mei 31, 2022

Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) imekubali kuwaachilia wanajeshi wawili wa Rwanda walioshikiliwa na DRC huku mivutano ikiongezeka kati ya majirani hao wawili, Rais wa Angola Joao Lourenco alitangaza Jumanne.

Tangazo hilo lilikuja baada ya Lourenco kufanya mazungumzo na Rais wa DRC, Felix Tshisekedi mapema Jumanne. Kutokana na ombi la mwenzake wa Angola, Rais Tshisekedi alikubali kuwaachia wanajeshi wawili wa Rwanda waliokamatwa hivi karibuni katika eneo la DRC, ofisi ya Lourenco ilisema.

Hatua hii ina azma ya kusaidia kupunguza mvutano katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili, iliongeza. Lourenco baadae alifanya mazungumzo kwa njia ya video na kiongozi wa Rwanda, Paul Kagame, Luanda ilisema.

Kufuatia mawasiliano tofauti na Lourenco, viongozi wa Rwanda na DRC walifikia maelewano ya kukutana ana kwa ana mjini Luanda katika tarehe itakayotangazwa baadae.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG