Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:15

Vifo vya raia na unyanyasaji wa haki za binadamu vinaongezeka nchini Mali


Ghasia za kisiasa nchini Mali zinasababisha ongezeka la vifo vya raia na unyanyasaji wa haki za binadamu nchini humo
Ghasia za kisiasa nchini Mali zinasababisha ongezeka la vifo vya raia na unyanyasaji wa haki za binadamu nchini humo

Vifo vya raia na manyanyaso ya haki za binadamu yanayofanywa na wanajeshi wa Mali yaliongezeka katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema Jumatatu lakini Bamako ilitupilia mbali shutuma hizo kuwa ni za upendeleo na ambazo hazijathibitishwa zilizolenga kulitia doa jeshi lake.

Wakati wanajihadi wakiendelea kuwa chanzo kikubwa cha ghasia dhidi ya raia kulikuwa na ongezeko kubwa la vifo na ukiukaji mwingine unaohusishwa na vikosi vya jeshi vinavyoungwa mkono na wanajeshi wa kigeni kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MINUSMA) kilisema.

Idadi ya watu waliouawa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 na pande zote katika mzozo; wanajihadi, wanamgambo, makundi yanayojilinda yenyewe, na vikosi vya usalama, iliongezeka mara nne katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ya mwaka 2021 kutoka 128 hadi 543.

Jumla ya vifo 248 vya raia vilitokana na vikosi vya ulinzi na usalama ripoti ilisema. Ilirekodi ukiukaji 320 wa haki za binadamu katika kipindi hiki ambacho kinaweza kulaumiwa kwa vikosi vya serikali ongezeko la mara kumi katika robo ya mwisho ya mwaka 2021 wakati kesi 31 zilinakiliwa.

XS
SM
MD
LG