Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 11:18

Mamia ya watu wameandamana DRC dhidi ya Rwanda kuliunga mkono kundi la M23


Waasi wa kundi la M23 nchini DRC

Mamia ya watu waliandamana dhidi ya Rwanda siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kinshasa kuhusu shutuma kuwa Kigali inaliunga mkono kundi la waasi la M23 huku mivutano kati ya majirani hao wawili ikiongezeka.

Waandamanaji hao pia walitoa wito wa kufukuzwa kwa balozi wa Rwanda nchini DRC na kubeba mabango yenye kuonyesha uzalendo wao. Congo ni nchi yetu, hakuna hata sentimita moja itakwenda Rwanda, moja ya bango lilisomeka hivyo.

Uhusiano umeingia dosari tangu kuwasili kwa idadi kubwa ya wahutu wa Rwanda huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo waliotuhumiwa kuwachinja watutsi wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Hata hivyo uhusiano ulianza kurejea katika hali nzuri baada ya Rais wa DRC, Felix Tshisekedi kuchukua madaraka mwaka 2019 lakini kuzuka upya hivi karibuni kwa ghasia za M23 kumezua hali ya wasiwasi iliyochangiwa na kuzuiliwa kwa wanajeshi wawili wa Rwanda nchini DRC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG