Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 11, 2024 Local time: 16:19

Mkuu wa jeshi la Sudan ameondoa hali ya dharura iliyowekwa tangu mapinduzi 2021


Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan akiwa kwenye mahojiano mjini Khartoum, Sudan, Dec 4, 2021.
Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan akiwa kwenye mahojiano mjini Khartoum, Sudan, Dec 4, 2021.

Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan siku ya Jumapili aliondoa hali ya dharura iliyowekwa tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021 baraza kuu linalotawala lilisema.

Burhan alitoa amri ya kuondoa hali ya dharura nchi nzima, baraza hilo lilisema katika taarifa yake. Agizo hilo lilitolewa ili kutayarisha mazingira ya mazungumzo yenye matunda na yenye maana ambayo yatafikia utulivu katika kipindi cha mpito, iliongeza taarifa.

Uamuzi wa Jumapili ulikuja baada ya mkutano na maafisa wa kijeshi kupendekeza hali ya hatari iondolewe na watu waliozuiliwa chini ya sheria ya dharura waachiliwe.

Pia imekuja baada ya wito wa karibuni uliotolewa na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa, Volker Perthes wa kuondoa hali ya dharura kufuatia mauaji ya waandamanaji wawili wakati wa maandamano yanayopinga mapinduzi hapo siku ya Jumamosi.

Sudan imekumbwa na maandamano makubwa tangu mapinduzi ambayo yamekabiliwa na msako mkali ambao umesababisha takribani watu 100 kuuawa na mamia kujeruhiwa kulingana na wahudumu wa afya wanaounga mkono demokrasia.

XS
SM
MD
LG