Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:47

Kampuni ya Nestle itasafirisha maziwa ya watoto kutoka Uswisi na Uholanzi kwenda Marekani


Kampuni ya Nestle ya Uswizi itasafirisha maziwa ya watoto kwenda Marekani kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo
Kampuni ya Nestle ya Uswizi itasafirisha maziwa ya watoto kwenda Marekani kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo

Kampuni kubwa ya chakula ya Uswisi ya Nestle itasafirisha maziwa ya watoto kutoka uswizi na Uholanzi hadi Marekani kufuatia uhaba wa maziwa uliopo msemaji wa kundi hilo alisema Jumanne.

Kampuni ya Uswizi itaingiza chapa mbili za maziwa yasiyo na athari za mzio kutokana na uhaba huo ambao umekuwa chanzo cha ziada cha msongo wa mawazo kwa wazazi wenye watoto wadogo wasiostahimili protini za maziwa ya ng’ombe.

“Tulizipa kipaumbele bidhaa hizi kwa sababu zinatumika kwa madhumuni muhimu ya matibabu” msemaji huyo aliliambia shirika la habari la AFP akithibitisha ripoti za vyombo vya habari.

Bidhaa hizi mbili tayari zimeagizwa kutoka nje; maziwa ya Gerber Good Start Extensive HA kutoka Uholanzi na maziwa ya Alfamino kutoka Uswizi. Ikikabiliwa na uhaba huo Nestle iliamua kusafirisha maziwa hayo kwa ndege ili kusaidia kukidhi mahitaji ya haraka lilisema kundi hilo ambalo pia lina viwanda viwili nchini Marekani vinavyozalisha maziwa ya watoto wachanga.

XS
SM
MD
LG