Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:23

Marekani inalaani shambulizi la Al-Shabaab lililopelekea vifo vya wanajeshi wa Burundi


Mfano wa mashambulizi yaliyofanywa na Al-Shabaab miaka michache iliyopita mjini Mogadishu. March 1, 2019
Mfano wa mashambulizi yaliyofanywa na Al-Shabaab miaka michache iliyopita mjini Mogadishu. March 1, 2019

Serikali ya Marekani imesema inasimama pamoja na Burundi wakati ikikabiliana na shambulizi la Al-Shabaab hapo Mei 3 kwa wanajeshi wa Burundi ambao wanahudumu katika kikosi cha mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) katika kambi huko Ceel-Baraf nchini Somalia.

Marekani kupitia taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje pia imetuma salaam za dhati za rambi rambi kwa familia za wanajeshi ambao walipoteza maisha katika shambulizi hilo ikiwemo wale waliojeruhiwa na waliopotea.

“Ujasiri wa wanajeshi wa Burundi kwa miaka mingi wamekuwa wakipambana dhidi ya ugaidi nchini somalia, Marekani bado itakuwa mstari wa mbele katika kuiunga mkono ATMIS na dhidi ya janga la ugaidi,” taarifa ilisema.

XS
SM
MD
LG