Mwanachama wa wanamgambo wa mrengo mkali wa kulia wa Oath Keepers siku ya Jumatano alikiri kushiriki katika njama za uchochezi wakati wa shambulizi la mwaka 2021 kwenye jengo la bunge la Marekani ikiwa ni ushindi wa karibuni kwa mahakama katika mifululizo ya kesi zinazoendelea huko.
William Todd Wilson wa jimbo la North Carolina alikiri mashtaka wakati mahakama ya serikali kuu ikisoma shtaka lake mjini Washington. Alikuwa mshtakiwa wa tatu wa Oath Keepers kukiri mashtaka ya kula njama ya uchochezi na kuingilia mashtaka.
Washitakiwa wengine kadhaa bado wako kwenye safu za kusomewa mashtaka baadae mwaka huu akiwemo Stewart Rhodes mwanzilishi wa Oath Keepers.
Mashtaka dhidi ya Rhodes na wengine ambayo hayajafunguliwa kuhusu tukio la Januari ndio kesi pekee ya uhalifu inayowashtaki washiriki katika shambulizi hilo la Januari sita mwaka 2021 la kushiriki katika njama ya uchochezi iliyofafanuliwa kama kujaribu kuipindua, kuiweka chini au kuiharibu serikali ya Marekani kwa kutumia nguvu.