Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:41

Wanajeshi wawili walevi huko DRC wameuwa raia 15 na kanali wa jeshi


Mfano wa wanajeshi wa Congo wakijiandaa kwa mazoezi huko North Kivu, Machi 2021
Mfano wa wanajeshi wa Congo wakijiandaa kwa mazoezi huko North Kivu, Machi 2021

Wanajeshi wawili waliokuwa wamelewa wamewaua kwa risasi watu 15 katika mashambulizi tofauti kwenye eneo tete la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) mamlaka ilisema Jumatatu.

Mwanajeshi mmoja aliyelewa aliwauwa abiria wanane na kuwajeruhi saba siku ya Jumatatu ndani ya boti kwenye ziwa Tanganyika, msimamizi wa eneo la Fizi katika jimbo la Kivu Kusini, Aime Kawaya Mutipula aliliambia shirika la habari la AFP. Waathirika wote ni raia, ni wanaume, wanawake na watoto, alisema.

Msemaji wa jeshi la eneo hilo Marc Elongo alisema mwanajeshi huyo Lukusa Kabamba wakati huo aliuawa na wakazi wenye hasira kabla hajakamatwa na kwamba alifariki kutokana na majeraha. Mratibu wa mashirika ya kiraia katika eneo hilo Andre Byadunia alisema awali kwamba mwanajeshi huyo aliwekwa rumande na aliisihi mamlaka kumpeleka mahakamani na kuhukumiwa.

Jumapili mwanajeshi mwingine alimfyatulia risasi na kumuua mlinzi wa kanali, kabla ya kumuua kanali wa jeshi pamoja na raia watano huko bamboo katika eneo la Djugu mamlaka ya eneo hilo ilitangaza katika mkoa wa Ituri.

XS
SM
MD
LG