Maafisa wa jimbo la South Carolina nchini Marekani wanasema wanachunguza tukio la ufyatuaji risasi katika klabu moja katika kaunti ya Hampton mapema Jumapili tukio ambalo lilisababisha watu tisa kujeruhiwa.
Ulikuwa ni ufyatuaji risasi wa tatu kwa umma nchini Marekani katika wikiendi ya sikukuu ya Pasaka. Matukio matatu ya ufyatuaji risasi huko South Carolina, Pittsburg na Pennsylvania yamesababisha vifo vya watoto wawili na takribani watu 31 kujeruhiwa.
Kitengo cha utekelezaji sheria cha jimbo la South Carolina ambacho kinachunguza tukio kwenye jimbo kilisema katika barua pepe kwamba hakukuwa na vifo vilivyoripotiwa katika ufyatuaji risasi wa mapema kwenye ukumbi wa Cara’s Lounge katika kaunti ya Hampton.
Hakuna taarifa zilizopatikana mara moja juu ya uzito wa majeraha hayo. Kaunti ya Hampton ipo takribani kilomita 129 sawa na maili 80 magharibi mwa mji wa Charleston.
Facebook Forum