Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:43

Mtaalamu wa UN anataka uchunguzi huru ufanyike mauaji ya Mali


Ukosefu wa usalama katikati mwa nchi ya Mali
Ukosefu wa usalama katikati mwa nchi ya Mali

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano alitoa wito wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu mauaji ya hivi karibuni katika eneo lililokumbwa na migogoro kati-kati mwa Mali.

Jeshi la Mali lilitangaza hapo April mosi kwamba limewaua wanamgambo 203 huko Moura kati-kati mwa taifa la sahel wakati wa operesheni yake mwishoni mwa mwezi machi. Hata hivyo tangazo hilo lilifuatia ripoti za mitandao ya kijamii zilizosambaa kwa wingi kuhusu mauaji ya raia katika eneo hilo.

Human Rights Watch pia ilisema wiki hii kwamba vikosi vya Mali na wapiganaji wa kigeni, waliwaua raia 300 huko Moura mwishoni mwa Machi, katika kile ilichokiita “unyama mbaya zaidi kuripotiwa katika mzozo wa silaha wa muongo mmoja nchini Mali”.

Siku ya Jumatano mtaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Alioune Tine alisihi ufanyike uchunguzi huru na usioegemea upande wowote kuhusu matukio hayo. Katika taarifa yake alitoa wito kwa mamlaka ya Mali kuruhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali unaojulikana kama MINUSMA kufanya uchunguzi.

XS
SM
MD
LG