Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 15:39

Benki kuu ya Zimbabwe imetangaza kupandisha viwango vya riba


Noti ya Zimbabwe
Noti ya Zimbabwe

Benki kuu ya Zimbabwe Jumatatu imetangaza kwamba imeongeza kiwango chake cha riba hadi asilimia 80 katika jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei uliofikia kiwango cha juu kutokana na athari za vita vya Ukraine.

Riba hiyo imeongezeka kutoka ile ya awali ya asilimia 60, iliyotangazwa mwezi Oktoba na ni riba ya juu sana duniani baada ya Venezuela na Argentina kulingana na vyanzo tofauti vya takwimu.

Hata hivyo mtandao wa Bloomberg unaofuatilia masuala ya kiuchumi na kifedha unasema riba hiyo ndiyo ya juu sana nchini humo tangu mwezi Septemba mwaka 2019 wakati benki kuu iliweka riba ya asilimia 70.

Mfumuko wa bei katika nchi hiyo yenye misukosuko ya kiuchumi ulipanda hadi asilimia 72.7 mwezi Machi kutoka asilimia 66.1 mwezi Februari.

XS
SM
MD
LG