Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 19:33

Biden amefanya mahojiano na majaji kupata mrithi wa Breyer


Rais wa Marekani, Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden amewafanyia mahojiano angalau wagombea watatu kwa nafasi ya jaji wa mahakama ya juu kulingana na mtu anayefahamu suala hilo huku White House inasisitiza kwamba bado anaendelea kufanya mchujo ili kuchagua mgombea wa mwisho ifikapo Jumatatu.

Msemaji wa White House, Jen Psaki alisema Jumanne kwamba Biden hajafanya uamuzi wa nani atakayemteua. Lakini Rais amewafanyia mahojiano majaji Ketanji Brown Jackson, J. Michelle Childs na Leondra Kruger kulingana na mtu anayefahamu suala hilo.

Mtu mwingine wa pili anayefahamu suala hilo pia alisema Rais Biden aliwahoji angalau wagombea watatu kwa nafasi hiyo. Watu hao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao kwa kujadili mchakati huu wa ndani.

Rais Biden ameahidi kuteua mwanamke wa kwanza mweusi katika mahakama kuu ifikapo mwishoni mwa mwezi huu ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kustaafu kwa Jaji Stephen Breyer. Haikuwa wazi ikiwa wagombea wengine wa ziada wamefanyiwa mahojiano na rais.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG