Upatikanaji viungo

Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 21:30

Jeshi la Nigeria limeua watoto katika shambulizi la anga huko Niger


Ramani ya Niger na nchi zinazopakana nazo

Jeshi la Nigeria limewaua na kuwajeruhi watoto katika shambulizi la anga kwenye nchi jirani ya Niger, kulingana na gavana wa eneo hilo nchini Niger, pamoja na televisheni ya taifa, na shirika la misaada walisema Jumapili ingawa vikosi vya jeshi vya Nigeria vilisema walikuwa bado wanafanya uchunguzi.

Shambulizi hilo lilitokea katika kijiji cha Nachade katika mkoa wa Maradi huko Niger siku ya Ijumaa kiasi cha kilomita chache kutoka mpaka na Nigeria alisema Chaibou Aboubacar gavana wa Maradi. Alisema watoto saba waliuawa na watano walijeruhiwa. Hakusema alijuaje kwamba vikosi vya Nigeria vilifanya shambulizi hilo.

Televisheni ya serikali ya Niger pia ilisema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na vikosi vya Nigeria bila kutoa ushahidi wowote. Kama suala la sera, jeshi la anga la Nigeria halifanyi uvamizi wowote katika maeneo yaliyo nje ya mipaka ya eneo la Nigeria. Hiyo ndio sera yetu Meja Jenerali Jimmy Akpor mkurugenzi wa habari za ulinzi wa Nigeria alisema. Aliendelea kusema kwamba uchunguzi ulikuwa unaendelea.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG