Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 02, 2022 Local time: 02:54

Morocco yafunga virago kombe la dunia


Swahili Morroco Kombe la Dunia

Morocco imekua timu ya pili ya Africa kuaga mashindano ya kombe la dunia baada ya kufungwa leo na Portugal bao 1-0. Cristiano Ronaldo ameipatia ushindi timu yake na kujiandikia mabao manne mpaka sasa katika michezo miwili. Morocco walipata nafasi nyingi za kuweza kupachika mabao lakini safu yao ya ushambuliaji ikawa butu. Morocco watakutana na Spain katika mechi yao ya mwisho ya mzunguko wa kwanza katika kundi B.

Misri ya Mohamed Salah, ni kama tayari imekwisha funga virago baada ya kupigwa jana na wenyeji Russia mabao 3-1. Mo Salah alifunga bao la penati la kufutia machozi. Russia tayari imekwisha jipatia tiketi ya kuingia kwenye mzunguko wa nane baada ya kushinda mechi zake mbili katika kundi A.

Mashabiki wa soka barani Africa wanaelekeza macho yao yote kwa timu ya Senegal ambayo ilifanya vizuri jana kwa kuichabanga Poland mabao 2 kwa 1.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG