Katika ujumbe wake wa Twitter amemuambia Rex “usitumiye nguvu zako bure,tutafanya kinachohitajika kufanywa.”
Wachambuzi wanasema haya yanatokana na kwamba siku ya Jumamosi wizara ya mambo ya nje ya Marekani kueleza kwamba Korea ya Ksakazini haijaonesha dalili za kutaka kuanza mazungumzo juu ya mipango yake ya silaha za nuklia na makombora.
Taarifa hiyo inafuatia matamshi ya Tillerson alipokua anakamilisha ziara yake ya Asia mjini Bejing, kukiri kwamba Marekani imekua ikiwasiliana moja kwa moja na Pyongyang.
Waziri huyo alikua China kujaribu kuirai kutumia ushawishi wake kuimwekea shinikizo Kim JOng Un kuacha majaribio yake na kuanza mazungumzo.