Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:48

Malumbano yagubika ufunguzi wa Bunge la Marekani


Spika Paul Ryan akiongoza sherehe za kuapishwa wabunge katika Baraza la Wawakilishi la 115.
Spika Paul Ryan akiongoza sherehe za kuapishwa wabunge katika Baraza la Wawakilishi la 115.

Malumbano yajitokeza siku ya kwanza ya Bunge jipya la Marekani Jumanne wakati wa-Republikani katika Baraza la Wawakilishi kupanga njama yao ya kwanza ya kubadilisha kanuni za ofisi ya maadili, lakini ghafla wakafuta mpango huo kufuatia malalamiko katika Bunge na kukemewa na Rais mteule Donald Trump.

Wa-Republikani walijiandaa kuchukua udhibiti kamili wa afisi huru isiyoegemea upande wowote ya kufuatilia maadili bungeni, hatua ambayo ingelipunguza uwezo wa afisi hiyo kuwachunguza wabunge ambao wanashukiwa kukiuka maadili au kutenda jinai.

Paul Ryan, Spika wa Baraza la Wawakilishi akifungua kikao cha Bunge
Paul Ryan, Spika wa Baraza la Wawakilishi akifungua kikao cha Bunge

Katika taarifa iliyokuwa ina unga mkono mabadiliko, Speaker wa Bunge Paul Ryan alisema afisi hiyo ya maadili inahitaji kufanyiwa mabadiliko “lakini akanang’ania” kuwa itaendelea kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa na kuhakikisha kwamba kuna uwajibikaji katika Congress.

Saa chacha baadaye, yeye spika na wafuasi wa Republikani bungeni walibadilisha msimamo wao wakati kelele za kupinga uamuzi huo zilipotinga kutoka pande zote mbili za Bunge.

“Hili ni jambo linatatiza sana na ni dalili mbaya ya matokeo yanayokuja, “Seneta mpya alieapishwa Chris Van Hollen aliiambia VOA.

XS
SM
MD
LG