Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:58

Mwanaharakati wa kiraia asema Sudan Kusini yatisha kwa mauaji.

Makazi ya maturubai ya watu waliokoseshwa makazi katika jimbo la Nuer sudan kusini
Makazi ya maturubai ya watu waliokoseshwa makazi katika jimbo la Nuer sudan kusini

Ahmed Bashir anasema zaidi ya wiki mbili sasa takriban watu wanne walipigwa risasi na kuuliwa nje ya mji wa Yambio.

Mwanaharakati wa kiraia Sudan Kusini katika jimbo la Gbuduwe anasema ghasia zimetanda katika mji wa Yambio.

Ahmed Bashir anasema zaidi ya wiki mbili sasa takriban watu wanne walipigwa risasi na kuuliwa nje ya mji wa Yambio.

Kamishna wa polisi katika jimbo la Gbuduwe anasema usalama umeongezwa katika eneo hilo.

Ahmed Bashir ni mwenyekiti wa taasisi ya kutetea haki za binadamu katika jimbo la Gbuduwe anasema mauaji ya hivi karibuni yaliyosababishwa na watu wasiojulikana yamepelekea wasiwasi mkubwa kwa wakaazi wa eneo hilo.

Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar akishikana mkono katika mkutano wa kwanza na rais Salva Kiir
Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar akishikana mkono katika mkutano wa kwanza na rais Salva Kiir

Anasema kuna mauaji mengi ndani ya nyumba za watu, licha ya kwamba kuna amani kidogo.

Makubalino ya amani yalifikiwa na vuguvugu la waasi la SSNLM na serikali lakini kuna hofu kubwa katika jumuiya zote . Mapema mwezi huu watu wasiojulikana waliokuwa na bunduki walimuuwa Rotto Zeni mwenye umri wa miaka 59 na mkewe Antonia Rotto mwenye umri wa miaka 55 katika mji wa Yambio. Rotto Zeni ni mmoja wa waandishi wa Azande na mwalimu wa siku nyingi katika jimbo la Equatorial.

Vijana wawili pia walipigwa risasi katika maeneo ya makazi ya Saura ambapo mmoja wao alikufa papo hapo. Mwingine alijeruhiwa vibaya na anatibiwa katika hospitali ya Yambio.

Bashir vametoa wito kwa maafisa wa jimbo kutekeleza makubaliano ya amani yaliyotiwa saini katika jimbo la Gbuduwe baina ya viongozi wa serikali na kundi la waasi linalojulikana kama Arrow boys.

XS
SM
MD
LG