Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 20:24

Watu 50 wauwawa katika klabu Orlando, Marekani


Meya wa Orlando Buddy Dyer, katikati, na mkuu wa polisi wa Orlando John Mina, kushoto, wawasili kuzungumza na waandishi habari kuhusu shambulizi la klabu ya Pulse Orlando Orlando, Fla., June 12, 2016.
Meya wa Orlando Buddy Dyer, katikati, na mkuu wa polisi wa Orlando John Mina, kushoto, wawasili kuzungumza na waandishi habari kuhusu shambulizi la klabu ya Pulse Orlando Orlando, Fla., June 12, 2016.

Mshambulizi mwenye asili ya Afghanistan amewauwa karibu watu 50 katika klabu moja ya usiku mjini Orlando, katika jimbo la Florida nchini Marekani, na kuwajeruhi zaidi ya wengine 50 kabla ya polisi kuvamia klabu hiyo na kuwaokoa walonusurika.

Afisa mmoja wa polisi aliyekua anafanyakazi kama mlinzi katika klabu hiyo ya Pulse, anasema alianza kufyetuliana risasi na mshambulizi karibu saa nane usiku, kabla ya mshambulizi kuwachukua mateka baadhi ya wateja wa klabu hiyo.

Tukio la shambulizi katika klabu Orlando
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:37 0:00

Maafisa wa usalama wakizungumza na waandishi habari Jumapili asubuhi wanamtaja mshambulizi kua ni Omar Saddiqui Mateen, ambae wazazi wake wanaotokea Afghanistan, na yeye alizaliwa Marekani.

Maafisa wa idara ya upelelezi wa masuala ya jinai hapa Marekani FBI, wanafanya uchunguzi na kulichukulia shambulizi hilo kama la kigaidi kwa wakati huu lakini hawana uhakika sababu za kushambuliwa kwa klabu hiyo inayowahudumia zaidi wapenzi wa jinsia moja.

Maafisa wanasema shambulizi hilo ndilo baya kabisa la mauwaji ya bunduki ya haliaki kutokea Marekani.

Mkuu wa Jamii ya Waislamu huko Florida ya kati Muhammad Musri amelaani kitendo hicho na kutoa wito kwa watu wote kuungana na kuwaombea waathiriwa, na kuomba kukomeshwa kwa mashambulizi ya halaiki yanayofanyika Marekani.

Shambulio hilo linafuatia jingine lillotokea katika mji huo siku moja kabla, pale muimbaji Christine Grimmie, kijana mwenye umri wa miaka 22, mashuhuri kwenye YouTube, alipouliwa alipokua anawapokea mashabiki wake baada ya kuimba.

Muimbaji wa The Voice Christina Grimmie
Muimbaji wa The Voice Christina Grimmie

.

XS
SM
MD
LG