Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:00

Majimbo ya Kentucky na Oregon yanajiandaa kupiga kura Jumanne


Wagombea urais wa Democrat, Hillary Clinton na Bernie Sanders.
Wagombea urais wa Democrat, Hillary Clinton na Bernie Sanders.

Wapigakura katika majimbo ya Kentucky na Oregon nchini Marekani wanajiandaa kupiga kura katika uchaguzi wa awali unaotarajiwa kufanyika Jumanne kwenye majimbo hayo.

Wagombea wawili wa urais wanaochuana kwenye chama cha Democrat bado wana wiki tatu za kampeni kabla ya kufanyika uchaguzi wa awali minne mbeleni ambayo itasaidia kuamua nani aendelee kubaki katika kinyang’anyiro hicho cha urais.

Wajumbe 213 wanatarajiwa kuchukuliwa katika uchaguzi huo wa awali wa mwezi Mei kabla ya kufikia uchaguzi wa awali katika jimbo la California unaosubiriwa kwa hamu ambapo kuna wajumbe 546 katika jimbo. Wakati waziri wa zamani wa mambo ya nje, Hillary Clinton anaongoza dhidi ya seneta wa Vermont, Bernie Sanders kwa takribani wajumbe 300 walioahidi kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi wa awali katika majimbo ya Kentucky na Oregon.

Seneta Sanders anaendelea kupata ushindi na anaahidi kuendelea kubaki katika kinyang’nyiro hadi mwezi Julai kwenye mkutano mkuu wa wajumbe wa chama cha Democrat unaotarajiwa kufanyika huko Philadeplhia.

Mgombea urais wa Republican, Donald Trump.
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump.

Kwa upande wa Republican, Donald Trump anaonekana kuwa ndie mgombea wa chama hicho, wakati timu ya Clinton ingependa kugeuza kampeni zao hivi sasa kuelekea ushindani katika uchaguzi mkuu, lakini hawawezi kufanya hivyo kutokana na kuwepo mpinzani hadi wakati huu ndani ya chama chake cha Democrat.

XS
SM
MD
LG