Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 07:24

Wapenda mageuzi Iran waongoza katika uchaguzi wa bunge


Kura zina hesabiwa kutokana na uchaguzi wa bunge wa Iran ulofanyika Ijuma Februari 26, 2016.
Kura zina hesabiwa kutokana na uchaguzi wa bunge wa Iran ulofanyika Ijuma Februari 26, 2016.

Wapenda mageuzi huko Iran wanaonekana wanapata ushindi katika uchaguzi wa bunge ulofanyika ijumaa, kutokana na ishara za matokeo ya awali yaliyotolewa Jumapili.

Wapenda mageuzi hao ambao wangelipendelea kuwa na ushirikiano zaidi na nchi za magharibi wamenyakua viti vyote 30 vya jimbo la Teheran.

Wapenda mageuzi Iran wapata ushindi katika uchaguzi wa bunge
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:27 0:00

Rais Hassan Rouhani na rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani wanaongoza pia katika uchaguzi wa wajumbe wa baraza la waatalamu, chombo chenye ushawishi mkubwa kinachofuatilia kazi za kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khameni, ambae ana kauli ya mwisho juu ya sera za kigeni za Iran na anaweza kumteuwa kiongozi ajae wa kidini.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:56 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Matokeo ya awali yanaonesha wagombea wa kihafidhina wakipoteza viti katika bunge la taifa lenye viti 290. Mwandishi habari wa Redio Iran Salim Saleh anasema matokeo ya safari hii yanaweza kuleta mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia nchini humo.

XS
SM
MD
LG