Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:40

Mashambulizi makali yazuka Bujumbura.


Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.

Serikali ya Burundi inadai kwamba washambuliaji 12 wamefariki dunia na watu wengine 21 kutekwa nyara, huku upande wa askari jeshi wa serikali watano wamejeruhiwa katika mapigano makali kuwahi kutokea tangu nchi hiyo ilipotumbukia katika mgogoro wa kisiasa mwezi April mwaka 2015.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:52 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Milio ya bunduki na milipuko imesikika alfajiri ya Ijumaa baada ya watu wenye bunduki kushambulia vituo viwili vya jeshi. Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameandika kwenye ukurasa wa tweeter kuwa mashambulio yalifanywa kwa lengo la kujaribu kuwaachia huru wafungwa waliokuwa kwenye kambi hizo za kijeshi.

Moja ya kambi iliyoshambuliwa ni ile la Ngagara, kaskazini mwa Bujumbura, lakini hakuna habari kamili zinazojulikana kuhusu tukio hilo.

Magari ya polisi na ya kijeshi yanashika doria katika mji wa Bujumbura huku kukiwa na raia wachache waliotoka nje.

Burundi imetumbukia katika mzozo wa kisiasa tangu mwezi April wakati Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwa atagombania mhula wa tatu na hatimaye kushinda katika uchaguzi.

Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba tangu kuanza kwa ghasia hizo takriban watu 240 wameuliwa na laki mbili kukimbia makazi yao na kwenda nchi za jirani.

Wakati huo huo mashirika ya ndege ya Kenya Airways na Rwanda Air yametangaza kusitisha safari zake kuelekea mji mkuu wa Bujumbura kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama katika mji mkuu huo.

XS
SM
MD
LG