Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:14

Buhari aamrisha kukamatwa kwa aliyekuwa mshauri wa usalama, Nigeria


Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria.
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ametoa amri ya kukamatwa kwa aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama nchini humo, kwa shutuma za kuiba mabilioni ya dola, fedha ambazo zilikusudiwa kununulia silaha za kupambana na kundi la Boko Haram.

Mashahidi wameiambia Sauti ya Amerika kwamba polisi wamezingira nyumba ya Sambo Dasuki katika mji mkuu, Abuja, na wamemzuia kutoka ndani licha ya jaji wa mahakama moja kusema kwamba Dasuki ana uhuru wa kusafiri ng’ambo kupata matibabu.

Dasuki alikuwa mshauri wa zamani wa Nigeria rais Goodluck Jonathan.

Serikali ya Nigeria ilisema Jumanne kwamba kati ya mwaka wa 2012 na 2015, Dasuki alitoa kandarasi za takriban dola bilioni mbili za kununulia ndege, mabomu na silaha zingine, vitu ambavyo havikupokelewa na jeshi la angani la Nigeria.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba kandarasi zingine za thamani ya dola bilioni mbili nukta nne hazikufaulu.

XS
SM
MD
LG