Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:37

Obama Aahidi Kusaidia Kuwasaka Washambulizi wa Paris


Rais Barack Obama, kushoto, na Rais Recep Tayyip Erdogan wap;iga picha baada ya mkutano wao mjini Antalya, Uturuki, Nov. 15, 2015.
Rais Barack Obama, kushoto, na Rais Recep Tayyip Erdogan wap;iga picha baada ya mkutano wao mjini Antalya, Uturuki, Nov. 15, 2015.

Rais Barack Obama wa Marekani ameapa Jumapili, kwamba ataisaidia Ufaransa katika juhudi za kuwasaka wahusika wa mashambulizi ya hivi karibuni mjini Paris yaliyosababisha vifo vya zaidi watu 100 na mamia wengine kujeruhiwa.

Baada ya kuwasili Uturuki kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la G20, Obama ameahidi ushirikiano na Ufaransa katika juhudi za kuwafikisha mbele ya sheria wote walohusika na mashambulizi hayo. Hakutoa maelezo zaidi juu ya jinsi Marekani au washirika wake wakaimarisha mashambulizi yao dhidi ya kundi la Islamic State lililodaia kuhusika na mashambulizi hayo.

"Mauwaji ya watu wasio na hatia, kwa msingi wa itikadi potofu, si shambulio dhidi ya Ufaransa pekee yake, sio tu dhidi ya Uturuki, bali ni shambulio kwa dunia iliyostarabika" alisema Obama baada ya kukutana kwa karibu saa moja na Rais Receop Tayyip Erdogan wa Uturuki.

XS
SM
MD
LG