Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:53

Watu 60 wauwawa Paris Katika Mashambulizi ya Kigaidi


Rescue workers and medics work by victims in a Paris restaurant, Nov. 13, 2015.
Rescue workers and medics work by victims in a Paris restaurant, Nov. 13, 2015.

Rais wa Ufaranca Francois Hollade aliondolewa kwa ghafla kutoka uwanja wa mpira wa Stade de France alipokua anatizama mchuano wa kandana kati ya Ufaransa na Ujerumani kutokana na milipuko miwili ya bomu karibu na uwanja huo.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinaripoti milipuko hiyo ni miongoni mwa mashambulio mengine matatu katika mji mkuu wa Ufaransa usiku wa Ijuma katika migahawa na Jumba la Sinema.

Watu 60 wanaripotiwa wameulwawa na haijulikani idadi ya majeruhi wakati hali ni ya wasi wasi. Kuna ripoti nyingine inayoeleza watu wengine 60 wanashikiliwa mateka katika jumba hilo la sinema, na mashahidi wanasema kuna hali ya taharuki ndani ya ukumbi huo.

Hadi hivi sasa haijulikani nani anaehusika na mashambulizi hayo yaliyotokea karibu wakati mmoja na wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema yamepangwa vizuri sana.

XS
SM
MD
LG