Bei za vyakula zimepanda kwa kiwango cha juu baada ya uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni nchini Tanzania.
Wiki moja baada ya wananchi wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo wa kihistoria, bado kunashuhudiwa kuzorota kwa baadhi ya huduma muhimu ikiwemo kuendelea kupanda kwa baadhi ya bidhaa hali ambayo inawakwaza wananchi wengi.
Hata hivyo, baadhi ya wadadisi wa mambo wanasema kuwa hali hiyo ni kawaida na bidhaa hizo zinatarajiwa kurejea kwenye bei yake ya kawaida katika kipindi kufupi kuanzia sasa.
Unga wa mahindi, mchele na sukari ni baadhi ya bidhaa zilizotajwa kuwa bei zake zimepanda sana.
“Nyama hivi sasa inauzwa shilingi 7,000 mpaka 8,000 kwa kilo, mara ya kwanza tulikuwa tunanunua shilling 6,000 buchani, hata mchele pia umepanda” alieleza mama mmoja wa nyumbani.
Ila kwa upande wa samaki bei ya kitoweo hicho inatajwa kuwa imebaki pale pale .