Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:12

Siku ya mashujaa yafana nchini Kenya


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Sherehe za mwaka huu za kuadhimisha mwaka 52 tangu uhuru zimefanyika katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi na kuhudhuriwa na halaiki kubwa ya watu-wakiwemo mashujaa waliopigania uhuru wan nchi hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Jumanne ameongoza taifa lake katika kuadhimisha mwaka wa 52 tangu nchi hiyo kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza.

Sherehe za mwaka huu za kuadhimisha mwaka 52 tangu uhuru zimefanyika katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi na kuhudhuriwa na halaiki kubwa ya watu-wakiwemo mashujaa waliopigania uhuru wan nchi hiyo. Vile vie sherehe hizo zimekuwa na shabaha ya kuwakumbuka mashujaa wa Kenya walio-peperusha bendera ya Kenya katika fani mbali mbali nchini na kwenye jumuiya ya kimataifa.

Siku ya mashujaa nchini Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:44 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kabla ya sherehe hizo, Rais Kenyatta alikagua gwaride la heshima kutoka kwa wanajeshi.

Baadaye Rais Kenyatta alizungumza kuhusu mafanikio ya Serikali yake tangu kuchukua hatamu ya uongozi.

Akizungumza kuhusu mashtaka yanayomkabili Naibu wake William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya ICC, Rais Kenyatta amewataka majaji wanao-sikiliza kesi hiyo kukoma kuingilia maswala ya ndani ya Kenya na hasa maombi yanayofanywa na wanasiasakumuombea William Ruto kwenye kesi inayomkabili ICC.

Vile vile RaisUhuru Kenyatta amegusiaswala nyeti la mswaada wa sharia wa kuwangandamiza waandishi wahabari uliopitishwa katika bunge hivi majuzi.

Mswaada huo wa vyombo vya habari umezusha taharuki kati ya waandishi wa habari-ambao wana-habari walikuwa tayari kwenda mahakamani kupinga kupitishwa kwa mswaada huo.

Lakini hotuba ya RaaisKenyatta imeshindwakuangazia maswalamenginemuhimu yanayokabili taifa kama vile mzozo wa mishahara kwa walimu,kuzorota kwa hali ya uchumi,ukosefu wa usalama.

Lakini jambo la kushangaza ni kwambahafla hiyo ya kitaifa haikuhudhuriwa naviongozi wote wa upinzani.

XS
SM
MD
LG