Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:41

Doria ya vikosi vya kijeshi Zanzibar yapokelewa kwa hisia tofauti.


Harakati za watu kwenye njia kuelekea mtaa wa Forodhani Unguja, Zanzibar
Harakati za watu kwenye njia kuelekea mtaa wa Forodhani Unguja, Zanzibar

Vikosi maalum vya majeshi na jeshi la Polisi vinaonekana katika mitaa mbali mbali ya kisiwa cha Unguja pamoja na hali kuonekana ni shwari na salama.

Lengo lao kuu ikiwa ni kuimarisha ulinzi lakini wakazi mbali mbali wa kisiwa hicho wana maoni tofauti Salum Mwalim ni naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar na mgombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Kikwajuni anasema hadhani hili ni suala la kulinda amani tu “angalia Tanganyika ina wakazi zaidi ya millioni 44 lakini huoni vikosi maalum huoni wanajeshi wakiranda randa mitaani..lakini ukija Zanzibar leo kila kona unakutana na askari...jambo ambalo linawajengea hofu wananchi.”

Vikosi vya usalama Zanzibar
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:42 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kwa baadhi ya wakazi wa upande wa Unguja wao walikuwa na maoni tofauti Hajji Suleiman mkazi wa Kilimani anasema inategemea na mazingira ya eneo na kwa eneo wanakoishi watu anaona ni mazuri na si mabaya ila kwa wengine askari wanaotembea mitaani si wazuri sana wanapiga watu bila kisa wakiwa wamekaa maskani.

Bolcher Juma anasema hawa ni kama watu wa kawaida wanaolinda ila hawajulikani wanalinda vipi maana wako kila mahali.

Ali Othmani Maulid anasema hii ni moja ya usalama wao kwasababu hata yeye atakuwa hana spidi ya kufanya tukio lolote kama kuna askari anayewalinda.

XS
SM
MD
LG