Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 08:27

Spika wa bunge la Marekani ajiuzulu


Picha ya Spika wa bungela Marekani John Boehner
Picha ya Spika wa bungela Marekani John Boehner

John Bohner spika wa Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani ametangaza kujiuzulu kutoka bungeni mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, tangazo ambalo limewashtusha wanasiasa na wananchi kwa ujumla.

Boehner, mbunge tangu mwaka 1990 amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka tawi la wenye siasa kali katika chama chake cha kihafidhina cha Republican kuhusu masuala kadhaa ya kisiasa na kijamii.

wadhifa wa spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani ni nafasi ya pili katika kuchukua uwongozi wa serikali ikiwa wote rais na makamu rais wanashindwa kuendelea na kazi zao.

Papa Francis akiwapungia mkono watu kutoka afisi ya Spika Bohner
Papa Francis akiwapungia mkono watu kutoka afisi ya Spika Bohner

Tangazo la Boehner limetolewa siku moja baada ya kumkaribisha Papa Francis kulihutubia bunge, ambapo alitoa wito kwa wabunge wote kuacha mivutano na kutekeleza kazi waliopewa na wapiga kura.

Boehner alichaguliwa na wabunge wenzake wa Republican kuwa spika karibu miaka mitano iliyopita na alijaribu kujiuzulu mwaka 2014 lakini kutokana na kushindwa kwa naibu wake Eric Cantor katika uchaguzi wa bunge aliamua kuendelea kubaki.

Akizungumza kutokana na tangazo hilo spika aliyemtangulia Mdemocrat Nancy Pelosi amesema uwamuzi huo unaonesha mvutano mkubwa ndani ya chama cha Repuclican kutokana na masuala mbali mbali yenye maslahi kwa wananchi.

XS
SM
MD
LG