Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:32

Bashir Aenda China Bila Kuogopa Kukamatwa na ICC


Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Ibrahim Ghandour, amesema mashtaka dhidi ya Rais Omar al Bashir, wa Sudan, yaliyowasilishwa mbele ya mahakama ya uhalifu wa kimataifa ya ICC huko The Hagiue ni tuhuma za nchi za ulaya pekee.

Bwana Ghandour, amesema mashtaka hayo yanapingwa na na jumuia nyingine za kimataifa ikiwa ni pamoja na viongozi wa umoja wa Afrika.

Waziri huyo alizungumza hayo kabla ya Rais Omar al Bashir kuelekea Beijing, China, kuanza ziara ya siku nne nchini China.

Akizungumza na sauti ya Amerika kwa njia ya simu, waziri Ghandour, amesema kuwa Rais Bashir, anendelea kutembelea nchi mbali mbali anazoalikwa na viongozi wenzake bila hofu ya kukamatwa.

Rais Bashir, Jumatatu ameanza ziara ya siku nne huko China chini ya mualiko wa serikali ya China kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya kushindwa kwa Japan katika vita ya pili vya dunia.

Hii ni ziara ya pili kwa kiongozi huyo wa Sudan kutembelea China. Waziri Ghandour, amesema kwamba Sudan na China zina uhusiano mzuri.

Ameongeza kusema, Sudan, ni miongoni mwa mataifa ya juu barani Afrika yenye ushirikiano mkubwa wa kiuchumi na China, na nchi hiyo iliisaidia Khartoum wakati wa kipindi kizito cha historia yake pale Marekani ilipoitenga.

Amesema ziara ya Rais Bashir, itakua ni pamoja na mazungumzo juu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, mkutano na wafanyabiashara wa China waliowekeza Sudan pamoja na watu kutoka Sudan wanoishi China.

Rais Bashir, alishitakiwa mwaka 2010 kwa uahlifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na vita ya jimbo la Darfur.

China haikutia saini mkataba wa kuundwa ICC lakini ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG