Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 00:44

Rais Nkurunzinza aapishwa.


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza akiapishwa kwa muhula wa tatu katika hafla bungeni mjini Bujumbura, Burundi, Alhamisi, Agosti. 20, 2015.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza akiapishwa kwa muhula wa tatu katika hafla bungeni mjini Bujumbura, Burundi, Alhamisi, Agosti. 20, 2015.

Ofisi ya rais wa Burundi imethibitisha kwamba rais Pierre Nkurunzinza ameapishwa kwa muhula wa tatu alhamisi katika hafla ya kushtukiza siku sita kabla ya tarehe iliyopangwa ya sherehe za kuapishwa.

Muhula wa tatu wa rais Nkurunzinza wa miaka mitano umekosolewa na baadhi kuwa unakiuka katiba na mkataba wa Arusha ambao ulimaliza rasmi vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 13 nchini Burundi.

Tangazo la rais Nkurunzinza la mwezi Aprili kwamba atagombea tena kwa muhula mwingine lilipelekea jaribio la mapinduzi na wiki kadhaa za maandamano ambapo zaidi ya watu 100 walifariki dunia.

XS
SM
MD
LG