Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 02:31

Kerry: kufanikisha mpango wa kimataifa wa nyuklia na Iran utaifanya dunia kuwa salama.


Mtangazaji wa VOA Setareh Derakhshesh akimhoji waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry katika wizara ya mambo ya nje. Julai 20, 2015.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alisema kufanikisha mpango wa kimataifa wa nyuklia na Iran utaifanya dunia kuwa salama zaidi, kuboresha maisha ya watu wa Iran na uwezekano wa kufungua fursa nyingine kati ya Marekani na Iran.

Katika mahojiano na VOA alisema ana matumaini waunga mkono watafanikiwa kuwashawishi watu kwamba makubaliano hayo yataizuia Iran kuweza kutengeneza silaha za nyuklia, kuzuia mizozo na kutoa usalama katika eneo hilo.

John Kerry
John Kerry

Bwana Kerry amekuwa akikutana na wabunge na kusema kwamba atawaambia ukweli mtupu kuhusu makubaliano hayo, katika kipindi cha siku 60 ambapo wabunge wanatathmini mkataba huo. Kerry alisema anatumaini wataona faida za makubaliano hayo na ana furaha kwamba wana miezi miwili ya kuutathmini mkataba kwa kina .“Nafikiri itawapa watu nafasi ya kutazama kwa undani na kuona kwamba kama usiporuhusu makubaliano haya unaweza kuwa unachagua kati ya vita na mapigano. Hilo ndio linaweza kuwa mbadala alisema".

Bunge lina uwezo wa kuidhinisha au kuukataa na lina uwezo wa kukataa kuondoa vikwazo vilivyowekwa na bunge. Rais wa Marekani, Barack Obama alisema anaweza kutumia kura ya turufu kwa hatua yeyote ya kupinga.

Mohammed Javad Zarif
Mohammed Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohamed Javad Zarif, waziri mwenzake bwana Kerry katika mashauriano yaliyochukua muda mrefu na kumalizika wiki iliyopita kwa makubaliano ya kihistoria ili kuzuia progam ya nyuklia ya Iran kwa mabadilishano ya kuwapa ahueni ya vikwazo, aliwasilisha waraka Jumanne kwa wabunge kwenye bunge la Iran, Majlis.

Baadhi ya wakosoaji wa mazungumzo hayo walisema Marekani ingeweza kusukuma kwa ajenda kubwa zaidi ikijumuisha masuala ya haki za binadamu, mageuzi ya kidemokrasia na kuachiwa huru kwa wamarekani kadhaa waliokamatwa nchini Iran.

Bwana Kerry alisema hali ya program ya nyuklia ya Iran ilikuwa lazima iwe kipaumbele cha kwanza lakini Marekani siku zote haiwezi kuacha kuamini demokrasia na haki za wananchi .Pia aliahidi kwamba serikali haitaacha kuzungumzia suala la wamarekani walio kizuizini.

“Lakini makubaliano haya yalihitaji kuondoa suala la nyuklia kwenye meza ya mazungumzo kwasababu tulikuwa tunatishwa na uwezekano wa hatari ya mashindano ya nyuklia katika eneo zima na hakuna anayefaidika na hilo.

Kerry alisema kwa hiyo ilibidi tuchague lililo muhimu. Tulilenga hilo la muhimu tumeondoa uwezekano wa mzozo kutokana na silaha za nyuklia ikiwa inakubalika na bunge na kukubaliwa na Majlis na kutekelezwa. Kama hilo likitokea nadhani dunia itakuwa salama zaidi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja makubalkiano hayo ya nyuklia.

Akiangalia siku zijazo Kerry alisema itakuwa miezi sita au zaidi kabla ya matokeo yoyote ya kuondoa vikwazo dhidi ya Iran kuonekana.

Pia kuna umuhimu wa kupitia tathmini ya bunge ambayo itaendelea mpaka mwezi Septemba. Na kwa Iran na taasisi ya kimataifa ya nishati ya Atomic (IAEA) kutafuta suluhu ya maswali juu ya mpango wa nyuklia wa Iran ifikapo mwishoni mwa Disemba.

Kama mpango huu ukipita na kukamilishwa watu wa Iran wataona maisha bora, wataona vikwazo vikiondolewa dhidi yao ambavyo vimezuia biashara, uwekezaji, na usafiri alisema bwana Kerry.

Kerry pia alizungumzia maelezo yaliyotolewa jumamosi na kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Khamenei ambaye alisema makubaliano ya nyuklia hayamaaninshi ushirikiano na Marekani katika masuala mengine na kuongeza kwamba Iran haita salimu amri kwa kile alichokiita matakwa mengi ya adui .

Waziri John Kerry (L) na Mohammad Javad Zarif
Waziri John Kerry (L) na Mohammad Javad Zarif

Kerry alisema taarifa hiyo ni mbaya sana na ya ajabu lakini anabaki na matumaini mazuri kuhusu masuala ya kidunia.“Kwa sasa hilo siyo tunaloliangalia alisema, tunalenga kuhusu makubaliano ya nyuklia na tutafanya tunachohitajika kufanya kuzuia shughuli nyingine kama tunafikiri zinaingiliana na usalama wa rafiki zetu na jamii yetu".

Hata hivyo kutokana na idadi ya mambo kadhaa yanayokumba dunia yetu, Kerry alisema wanadiplomasia hawana nafasi ya kuangalia jambo moja pekee bila kufanya kitu kuhusu mengine.

“Huwezi kudharau yanayotokea nchini Syria, huwezi kudharau yanayotokea Iraq au Yemen au Misri au Sinai alisema. Haya mambo yote yanaingiliana na sisi tunaoshughulika na diplomasia na maisha ya umma katika dunia ya leo tuna picha ngumu sana tunayojaribu kuiunganisha".

Alisema kuweka haya mambo yote pamoja si rahisi lakini masuala hayo yatasuluhishwa na makubaliano kama yale ambayo yaliafikiwa na Marekani, China, Ufaransa, Russia na Ujerumani pamoja na Iran.

Lakini lazima tuyapiganie alisema Kerry.

XS
SM
MD
LG