Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 27, 2021 Local time: 15:03

Maiti ya Kijana wa Liberia Yakutwa na Ebola


Picha ya mfano wa virusi vya Ebola

Mwili wa kijana na Liberia mwenye umri wa miaka 17 aliyekufa, umepimwa na kukutwa na virusi vya Ebola.

Ugunduzi huo unafanya kuwa maambukizi ya kwanza tangu nchi hiyo kutangaza kumalizika kwa maambukizi ya ugonjwa huo Mei 9.

Naibu waziri wa afya wa Liberia, Tolberth Nyenswah, amesisitiza Jumanne, kwamba hakuna sababu ya kuwa na wasi wasi.

Amesema mwili wa kijana huyo ulizikwa kwa usalama na timu ya kufuatilia walio karibu na marehemu imeshaanza kufanya kazi.

Shirika la AP linaripoti kwamba kijana huyo alifariki Juni 24, katika wilaya ya Magharibi karibu na mapka wa Sierra leone na Guinea.

Mataifa hayo ni mataifa mawili yaliyoathiriwa vibaya na ugonjwa huo wakati wa mlipuko ulioanza kwisha.

Ona maoni (1)

mjadala huu umefungwa
XS
SM
MD
LG