Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:19

ISIS Yawakata Wanawake Vichwa


Wanaharakati wa Syria, wamesema wanamgambo wa Islamic State, wamewakata vichwa wanawake nchini humo kwa mara ya kwanza.

Shirika la ufuatiliaji wa haki za binadamu nchini Syria, lenye makao yake Uingereza limesema leo Jumanne kwamba wanawake hao walikatwa vichwa pamoja na waume zao.

Tukio hilo lilitokea kwenye jimbo la mashariki la Deir Ezzor, huko Syria baada ya kushutumiwa kufanya uchawi.

Shirika hilo linalofuatilia ghasia nchini Syria kupitia mtandao wa vyanzo vya ndani limesema wanamgambo wa Islamic state wameuwa zaidi ya watu elfu tatu huko Syria.

Mauaji hayo yamefanyika tangu ilipojitangazia kile ilichokiita umilki, mwaka mmoja uliopita ikiwemo karibu raia 1,800.

Kukatwa vichwa kama sehemu ya mauaji siyo jambo jipya katika kundi hilo ambalo limefanya matukio kama hayo kwa raia wa Syria, pamoja na waandishi wa habari na wafanyakazi wa kigeni.

XS
SM
MD
LG