Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:25

Watu 23 Wauwawa nchini Chad


Watu 23 wameuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya pamoja ya kujitoa muhanga yaliyowalenga polisi katika mji mkuu wa Chad.

Serikali ya nchi hiyo imewanyoshea kidole wanamgambo wa Boko Haram kwa umwagaji huo wa damu kwa mujibu wa shirika la habari AFP.

Kulikuwa na mashambulizi kama hayo katika mji mkuu wa nchi hiyo iliyopo Afrika ya kati ambayo ipo mstari wa mbele katika mapambano ya kikanda na kundi la Boko Haram.

Serikali katika taarifa yake, imeeleza kwamba wanamgambo hao wamefanya mashambulizi katika eneo hatari kwa kufanya unyama wao, na watasakwa na kumalizwa popote pale walipo.

Imeeleza pia watu 23 waliuwawa na wengine 101 kujeruhiwa katika mashambulizi mfululizo nje ya makao makuu ya polisi na chuo cha polisi mjini N’Djamena.

XS
SM
MD
LG