Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 19:54

Marekani imejiandaa kupeleka washauri wa kijeshi Iraq.


Wanajeshi wa Iraqi wakifanya mafunzo yanayoongozwa na Marekani huko kwenye kambi ya Taji, Iraq, Juni 2, 2015.
Wanajeshi wa Iraqi wakifanya mafunzo yanayoongozwa na Marekani huko kwenye kambi ya Taji, Iraq, Juni 2, 2015.

Marekani imeonekana imejiandaa Jumatano kupeleka washauri wa kijeshi wapatao 400 huko Iraq katika juhudi mpya ya kuimarisha vikosi vya Iraq wakati vikijaribu kuikomboa Ramadi , makao mkuu ya jimbo la Anbar lililotekwa mwezi uliopita na kundi la Islamic State.

Washauri hao wa ziada wanaongezwa katika kundi la wengine 3,100 ambao tayari wako Iraq lakini rais wa Marekani Barack Obama bado anaendelea kufuta uwezekano wa kupeleka majeshi ya askari wa miguu nchini Iraq baada ya kuyaondoa mwaka 2011.

Marekani wanatarajia kufungua kituo kipya cha mafunzo huko al-Taqqadum eneo la anga la jangwani ambalo wakati fulani lilikuwa kituo cha jeshi la Marekani

XS
SM
MD
LG