Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 09:38

Spika wa Zamani wa Marekani Akana Mashitataka


Spika wa zamani wa Bunge la Marekani, kutoka chama cha Repablikan, Dennis Hastert, amekana mashitaka katika mahakama kuu ya Marekani.

Bwana Hastert, anakabiliwa na makosa ya uvunjifu wa taratibu za kibenki na kudanganya idara ya upelelezi ya makosa ya jinai ya Marekani FBI.

Akiwa na umri wa miaka 73, Hastert aliwahi kuwa kwenye nafasi ya pili katika urithi wa urais, alitakiwa kuwasilisha pasi yake ya kusafiria na kurudisha silaha yoyote ya moto aliyokuwa nayo nyumbani kwake.

Muwakilishi huyo wa zamani wa jimbo la Illinois, anatuhumiwa kwa kutoa mamia ya maelfu ya dola kutoka katika akaunti yake ya benki kwa kile taarifa za vyombo vya habari zinazoeleza ni za kunyamazisha tuhuma za kuwadhalilisha watu kijinsia.

XS
SM
MD
LG