Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:27

Mafuriko ya Dar yawakosesha makazi maelfu ya watu


Tanzania floods
Tanzania floods

Hali ya wasi wasi inawakumba sehemu kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam kutokana na mfuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kutokana na hali hiyo serikali imewashauri wakazi wa jiji hilo kuu la biashara Tanzania, kuelekea maeneo ya nyanda za juu na kutoka maeneo ya mabonda.

Maafisa wanasema wanafanya kila wawezalo kuwasaidia wanohitaji msaada baada ya kukoseshwa makazi, lakini hawajaweza kuthibitisha idadi ya watu waloathiriwa na walofariki. vyombo vya habari vinatoa idadi zinazotofautiana kati ya mtu moja kufariki hadi wanne.

Wakazi wa Dar Es Salaam wakizungumza na Sauti ya Amerika wanaulaumu uzembe wa serikali kwa mafuriko hayo, huku wengine wakidai ni ukosefu wa miundo mbinu madhubuti kuweza kuruhusu maji kupita katika mitaro bila ya tatizo.

XS
SM
MD
LG