Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 14:45

Upinzani Congo uko tayari kukutana na rais Kabila.


Rais Joseph Kabila akiwa na Rais Obama na mkewe Michelle, huko White House.
Rais Joseph Kabila akiwa na Rais Obama na mkewe Michelle, huko White House.

Viongozi wa upinzani nchini DRC wameeleza kwamba wako tayari kwa mazungumzo na Rais Joseph Kabila kabla ya kufanyika uchaguzi, wakiserma jambo hilo huwenda likasaidia kuepuka migogoro wakati wa uchaguzi.

Matamshi hayo yametolewa kufuatia ripoti kwamba Rais Kabila yuko tayari kuzungumza na upinzani juu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Mwakilishi wa chama cha UDPS Ribes Mikindo, alithibitisha kuwepo na ripoti hiyo alipozungumza na VOA, akieleza kwamba jambo kubwa litakuwa kuona ni jinsi gani uchaguzi wa nchi utaweza kufanyika ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa wabunge .

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Kambale Mota huko mashariki ya mwa Congo amesema mawasiliano kati viongozi wan chi hiyo ni jambo jema lakini pia inaweza kuwa shida ikiwa watakwenda kinyume cha katiba na maslahi ya wakazi wa Congo.

Uchaguzi mkuu wa Congo unatazamiwa kufanyika baadae mwaka 2016, na upinzani unapinga kwa Rais Kabila kugombania mhula mwengine kwani inakwenda kinyume na katiba ya nchi.

XS
SM
MD
LG