Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 07:23

Viongozi wa dunia walaani shambulio la Tunis


Watunisia wakiwasha mishuma kwenye mlango mkuu wa Jmba la Makumbusho ambako watu waliuliwa Jumatano.

Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi, aliwatembelea waathiriwa wa shambulio la jumatano baada ya washambuliaji kuvamia Jumba la Makumbusho la Tunisia, Bardo, na kuwauwa watali 17 wakigeni na Watunisia wawili, katika shambulizi baya la kigaidi kutokea nchini humo katika kipindi cha muongo mmoja.

Rais Essebsi alipokelewa hospitali na waziri wa utali Salma Elloumi, na kuwatembelea baadhi ya walojeruhiwa na kukutana na wafanyakazi wa hospitali na kusema .

“Hatujapata kushuhudia ugaidi hapa Tunisia, hii imetoka nje.”

Watu 44 walijeruhiwa wakati washambuliaji wakiva mavazi ya kijeshi walishambulia Jumba la Taifa la Makumbusho la Tunisia siku ya Jumatano.

Watali walouliwa ni pamoja na watano kutoka Japan, wanne kutoka Utaliana, wawili wa Colombia, wawili kutoka Hispania, pamoja na Mfaransa, Maustralia na raia wa Poland.

Muathiriwa wa shambulio la jumba la makumbusho la Bardo, Tunis, Tunisia.
Muathiriwa wa shambulio la jumba la makumbusho la Bardo, Tunis, Tunisia.

Wageni kadhaa walikimbilia ndani ya jengo wakati wa shambulio hilo na wanamgambo ambao maafisa wa usalama hawakuwatambulisha, waliwashika watu mateka ndani.

Maafisa wa usalama walingia ndani ya jumbe hilo saa mbili baada ya kuanza shambulio na kuwauwa washambulizi wawili na kuwaokowa wote walokuwa wanashikiliwa mateka.

Shambulio hilo lililolenga shabaha muhimu kama hiyo, ni pigo kwa taifa dogo la Afrika Magharibi linalotegemea sana watali kutoka Ulaya ambalo limeweza kunusurika kwa kutokumbwa na ghasia za wanamgambo kama mataifa jirani, tangu kuanza kwa mapinduzi yaliyomuondowa madarakani rais wa muda mrefu Zine El-Abidine Ben Ali.

Viongozi wa kimataifa wamekuwa wakituma salamu za uungaji mkono na rambi rambi kwa wa-Tunisia.

Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama, alitoa risala za rambi rambi akiwa Tokyo, alipokua anahutubia katika sherehe za kuzindua mpango wa pamoja kati ya Marekani na Japan wa kuimarisha elimu kwa ajili ya wasichana.

“Kabla ya kuanza kwa niaba yangu na mumewangu ninataka kuungana na wengine kutoa rambi rambi rambi zetu kutokana na tukio la kikatili huko Tunisia. Dua zetu ziwafikiye familia za waathiriwa wa hapa Japan na kwengineko duniani,” amesema Bi. Obama

Kabla ya hapo waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, alilaani vikali shambulizi hilo la Tunis alipowasili kazini na kuzungumza na waandishi habari.

“Tunafanya kila tuwezalo kuweza kuthibitisha mahala raia wa Japan waliko huko Tunis. Kwa wakati huu tuna habari kwamba takriban raia wetu watatu wameuliwa na watatu wamejeruhiwa." alisema Bw. Abe.

Maafisa wa usalama wa Tunisia wanasema wanawatafuta watu wengine watatu wanaodhaniwa walihusika na shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG