Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:23

Marekani kulegeza vikwazo dhidi ya Sudan.


Donald Booth, mwakilishi maalum wa Marekani nchini Sudan na Sudan Kusini akiongea na waandishi wa habari mjini Juba.

Marekani ilisema Jumanne kuwa inapunguza vikwazo vya muda mrefu vilivyowekwa dhidi ya nchi ya Sudan na hivyo kuruhusu wamarekani kupeleka vifaa mbali mbali vya mawasiliano ikiwa ni pamoja na simu na kompyuta ya mkononi.

Wizara ya fedha ya Marekani ilisema mabadiliko hayo yanafanyika mara moja na kwamba yanaruhusu uuzaji wa radio na kamera za dijitali.

Donald Booth mwakilishi maalum wa Marekani nchini Sudan na Sudan Kusini aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba mabadiliko juu ya vikwazo hivyo yanafuatia ahadi ya utawala wa Sudan kuruhusu uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya mawasiliano.

Alisema mabadiliko hayo pia yanalenga kuwasaidia raia wa Sudan kujiunga katika dunia ya mtandao wa dijitali.

XS
SM
MD
LG