Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 08, 2022 Local time: 01:44

Umoja wa Mataifa wakemea shambulizi la Libya.


Hoteli ya Cortinthia ikiwa inaungua baada ya shambulizi huko Tripoli, Libya, Jumanne, Jan. 27, 2015.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na washiriki wa mazungumzo ya amani yanayodhaminiwa na Umoja huo wamekemea shambulizi la Jumanne katika hoteli ya kifahari mjini Tripoli, Libya, na kuua watu tisa.

Taarifa ya Baraza la Usalama imetoa mwito kwa pande zote nchini Libya, kuwa sehemu ya juhudi za kuzungumzia matatizo ya kisiasa na usalama yanayo ikabili nchi hiyo, ambayo imekuwa katika wakati mgumu wa hali thabiti toka kuondoka kwa kiongozi wa zamani Moammar Gadhafi.

Baada ya siku mbili za mazungumzo mazuri yenye kujenga mjini Geneva, Uswisi, Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Libya, imesema mashambulizi ya kama Jumanne hayatawezesha shughuli za kuelekea kupatikana kwa serikali ya umoja, bali yatakuwa kichocheo cha pande zote za Libya kuendeleza hali ya taharuki.

XS
SM
MD
LG